BODABODA WANAVYOITIA HASARA HOSPITALI YA BUGANDO
Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza. HOSPITALI ya rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza imekuwa ikipata hasara ya takribani Sh. milioni tano mpaka milioni 12 kila wiki ikiwa ni misamaha ya gharama za matibabu ya majeruhi wa ajali za barabarani hususani bodaboda. Katika mahojiano maalumu na mwandishi, Afisa Ustawi wa Jamii hospitali ya Bugando, Daudi Makumucha, alisema, “Gharama kubwa za matibabu zinawatesa majeruhi wengi wanofikishwa hospitalini. “Wapo wanaolazimika kuuza mali zao ili aweza kumudu gharama za matibabu.” Alisema hali hiyo inailazimu hospitali hiyo kutoa msamaha wa matibabu kila wiki kwa wagonjwa ambao hawana uwezo wala ndugu wa kumudu kulipa gharama hizo. “Leo pekee (Julai 13, 2017) tumejadili mafaili ya wagonjwa kumi na kupitisha msamaha wa madeni kiasi kinachofikia shilingi milioni tano,….kuna mgonjwa kutoka wodi ya mifupa, alipata ajali na alikuwa anadaiwa takribani Sh. 2,474,800/-” alisema. Kwa mujibu wa Makumucha, majeruhi h...