Posts

Showing posts from August, 2017

Boda boda;Kundi linaloonekana kuwa sugu kwa kutofuata sheria za usalama barabarani

Image
Kundi linaloonekana kuwa sugu kwa kutofuata sheria za usalama barabarani ni waendesha pikipiki halimaaarufu kama bodaboda. Kero kubwa imekuwa kutovaa kofia ngumu (helmets) pamoja na abiria wao, kukimbiza pikipiki kupita kiasi, kutotii maelekezo ya taa za barabarani kwa wale wanaotumia barabara zenye huduma za taa elekezi. Wakati mwingine hufanya makusudi kwa kujiamini kukimbia ama kulipa faini. Kwa utafiti uliofanywa na blogu hii, Licha ya bodaboda hao kutotii sheria bila shuruti, lakini pia abiria wa usafiri huu wanaonekana kuwa wagumu kutumia kofia hizi, hasa wanawake kwa kudaidi ni chafu ama kuharibu mitindo yao ya nywele. Baadhi ya bodaboda wachache wanakubaliana na adhabu kuwepo kama vile kutembezwa barabarani wakiimba nyimbo, au kuchuchumaa, kama njia mojawapo ya kuwarekebisha,  japo wapo wanaodai ni uvunjifu wa haki za binadamu. Akiongea na blogu hii Inspekta Hassan Makame mkuu wa askari kikosi cha usalama barabarani eneo la Mwenge jijini Dar es salaam, kwa kiten...

AJALI ZA BODA BODA

Inakadiriwa kwa siku hospitali ya taifa ya muhimbili,inapokea majeruhi takribani 30 mpaka 50 kwa siku wanaotokana na ajali za boda boda ndani ya jiji la Dar es Salaam. Maneno hayo yalisemwa na Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani Tanzania. (ACP. Theopista Mallya)