Boda boda;Kundi linaloonekana kuwa sugu kwa kutofuata sheria za usalama barabarani

Kundi linaloonekana kuwa sugu kwa kutofuata sheria za usalama barabarani ni waendesha pikipiki halimaaarufu kama bodaboda. Kero kubwa imekuwa kutovaa kofia ngumu (helmets) pamoja na abiria wao, kukimbiza pikipiki kupita kiasi, kutotii maelekezo ya taa za barabarani kwa wale wanaotumia barabara zenye huduma za taa elekezi. Wakati mwingine hufanya makusudi kwa kujiamini kukimbia ama kulipa faini.

Kwa utafiti uliofanywa na blogu hii, Licha ya bodaboda hao kutotii sheria bila shuruti, lakini pia abiria wa usafiri huu wanaonekana kuwa wagumu kutumia kofia hizi, hasa wanawake kwa kudaidi ni chafu ama kuharibu mitindo yao ya nywele.
Baadhi ya bodaboda wachache wanakubaliana na adhabu kuwepo kama vile kutembezwa barabarani wakiimba nyimbo, au kuchuchumaa, kama njia mojawapo ya kuwarekebisha,  japo wapo wanaodai ni uvunjifu wa haki za binadamu.

Akiongea na blogu hii Inspekta Hassan Makame mkuu wa askari kikosi cha usalama barabarani eneo la Mwenge jijini Dar es salaam, kwa kitendo alichokifanya cha kuwakamata na kuwaimbisha  bodaboda (Kutafuta kiki kwa pikipiki) waendeshaji wasiokuwa na leseni, kofia ngumu za kichwani na wanaoendesha bila kufuata taratibu za usalama barabarani kwa ujumla, yeye anasema lengo sio kukomoa wala kudharirisha kama baadhi walivyopokea, bali kuwakumbusha wajibu wao wawapo barabarani.

Comments

Popular posts from this blog

BODABODA WANAVYOITIA HASARA HOSPITALI YA BUGANDO

AJALI ZA BODA BODA