Posts

BODABODA WANAVYOITIA HASARA HOSPITALI YA BUGANDO

Image
Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza. HOSPITALI ya rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza imekuwa ikipata hasara ya takribani Sh. milioni tano mpaka milioni 12 kila wiki ikiwa ni misamaha ya gharama za matibabu ya majeruhi wa ajali za barabarani hususani bodaboda. Katika mahojiano maalumu na mwandishi, Afisa Ustawi wa Jamii hospitali ya Bugando, Daudi Makumucha, alisema, “Gharama kubwa za matibabu zinawatesa majeruhi wengi wanofikishwa hospitalini. “Wapo wanaolazimika kuuza mali zao ili aweza kumudu gharama za matibabu.” Alisema hali hiyo inailazimu hospitali hiyo kutoa msamaha wa matibabu kila wiki kwa wagonjwa ambao hawana uwezo wala ndugu wa kumudu kulipa gharama hizo. “Leo pekee (Julai 13, 2017) tumejadili mafaili ya wagonjwa kumi na kupitisha msamaha wa madeni kiasi kinachofikia shilingi milioni tano,….kuna mgonjwa kutoka wodi ya mifupa, alipata ajali na alikuwa anadaiwa takribani Sh. 2,474,800/-” alisema. Kwa mujibu wa Makumucha, majeruhi h...

'WANASIASA WANAWAPA KIBURI BODABODA MBEYA"

Image
Na Adrian Mgaya. Baadhi ya madereva wa pikipiki na bajaj mkoani Mbeya ambao wengi wao wana umri chini ya miaka 35, wapo katika hatari ya kupata madhara yatokanayo na athari za ajali za barabarani kutokana na kuwa wakaidi kwa mamlaka zinazosimamia usalama barabarani. Butusyo Akimu Mwombelo ambaye ni mkuu wa kikosio cha usalama barabarani mkoa wa Mbeya anasema, ongezeko kubwa la ajali za barabarani linachochewa na madereva wa pikipiki na bajaj. Hata hivyo juhudi za kupambana na hali hiyo zina vikwazo vingi kutokana na mwingiliano na mambo ya siasa. Tazama video hii kufahamu zaidi.

Boda boda;Kundi linaloonekana kuwa sugu kwa kutofuata sheria za usalama barabarani

Image
Kundi linaloonekana kuwa sugu kwa kutofuata sheria za usalama barabarani ni waendesha pikipiki halimaaarufu kama bodaboda. Kero kubwa imekuwa kutovaa kofia ngumu (helmets) pamoja na abiria wao, kukimbiza pikipiki kupita kiasi, kutotii maelekezo ya taa za barabarani kwa wale wanaotumia barabara zenye huduma za taa elekezi. Wakati mwingine hufanya makusudi kwa kujiamini kukimbia ama kulipa faini. Kwa utafiti uliofanywa na blogu hii, Licha ya bodaboda hao kutotii sheria bila shuruti, lakini pia abiria wa usafiri huu wanaonekana kuwa wagumu kutumia kofia hizi, hasa wanawake kwa kudaidi ni chafu ama kuharibu mitindo yao ya nywele. Baadhi ya bodaboda wachache wanakubaliana na adhabu kuwepo kama vile kutembezwa barabarani wakiimba nyimbo, au kuchuchumaa, kama njia mojawapo ya kuwarekebisha,  japo wapo wanaodai ni uvunjifu wa haki za binadamu. Akiongea na blogu hii Inspekta Hassan Makame mkuu wa askari kikosi cha usalama barabarani eneo la Mwenge jijini Dar es salaam, kwa kiten...

AJALI ZA BODA BODA

Inakadiriwa kwa siku hospitali ya taifa ya muhimbili,inapokea majeruhi takribani 30 mpaka 50 kwa siku wanaotokana na ajali za boda boda ndani ya jiji la Dar es Salaam. Maneno hayo yalisemwa na Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani Tanzania. (ACP. Theopista Mallya)